1 Chronicles 2:3-15

Yuda

Hadi Wana Wa Hesroni

3 aWana wa Yuda walikuwa:
Eri, Onani na Shela. Hawa watatu walizaliwa kwake na mkewe Mkanaani, binti wa Shua. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa Bwana, kwa hiyo Bwana alimuua.
4 bTamari, mkwewe Yuda, alimzalia wana wawili: Peresi na Zera. Yuda alikuwa na jumla ya wana watano.

5 cWana wa Peresi walikuwa:
Hesroni na Hamuli.
6 dWana wa Zera walikuwa:
Zimri, Ethani, Hemani, Kalkoli na Dara. Jumla ya wana wa Zera walikuwa watano.
7 eMwana wa Karmi alikuwa:
Akari,
Akari maana yake Taabisha; pia anaitwa Akani (Yos 6:1-26; 22:20).
ambaye alileta taabu kwa Waisraeli kwa kukiuka onyo la kutokuchukua vitu vilivyokuwa vimewekwa wakfu.
8Mwana wa Ethani alikuwa:
Azariya.
9 gWana wa Hesroni walikuwa:
Yerameeli, Ramu na Kalebu.

Kuanzia Ramu Mwana Wa Hesroni

10 hRamu alimzaa
Aminadabu, na Aminadabu akamzaa Nashoni, kiongozi wa kabila la Yuda.
11Nashoni akamzaa Salmoni, Salmoni akamzaa Boazi, 12 iBoazi akamzaa Obedi, Obedi akamzaa Yese.
13 jYese akawazaa
Eliabu mwanawe wa kwanza; wa pili Abinadabu, wa tatu Shimea,
Au: Shima, maana yake Sifa njema (pia 1Sam 16:9; 17:13).
14wa nne Nethaneli, wa tano Radai, 15wa sita Osemu, na wa saba Daudi.
Copyright information for SwhNEN